Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ole Hali Mbaya Man United

0 Ole Gunnar Solskjaer Ole Hali Mbaya Man United

Mon, 25 Oct 2021 Chanzo: globalpublishers.co.tz

#OleOut ndio hashtag inayosambaa katika mtandao wa kijamii wa Twitter mara baada ya Manchester United kupokea kipigo kizito cha mabao 5-0 kutoka kwa Liverpool katika uwanja wao wa Nyumbani ‘Old Trafford’.

Hashtag hiyo ikiwa ni sehemu ya ukutaka Uongozi wa klabu hiyo kumfuta kazi kocha Ole Gunnar Solskjaer kutokana na matokeo mabaya ambayo timu hiyo imekuwa ikipata katika michezo ya hivi karibuni.

“Haiwezekani Ole kuendelea kuwa kocha, muda wa kufutwa kazi imefika sasa” alisema mmoja wa mashabiki wa klabu hiyo katika mtandao wa Twitter.

United mpaka sasa imecheza mechi 9 wakiwa nafasi ya 7 katika msimamo wa Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) wakishinda mechi nne, wakitoka sare mechi mbili na kupoteza mechi tatu huku wakifunga jumla ya mabao 16 na kuruhusu kufungwa mabao 15.

Chanzo: globalpublishers.co.tz