Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Okwi aitwa Uganda Cranes kuikabili Taifa Stars Afcon

12410 Pic+okwi TanzaniaWeb

Fri, 17 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Kampala, Uganda. Mshambuliaji mahiri wa Simba, Emmanuel Okwi, ameitwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Uganda ‘The Cranes’ inayojiandaa kucheza na Taifa Stars, mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Mataifa Afrika.

Okwi amejumuishwa kwenye kikosi cha nyota 30 watakaoingia kambini Septemba Mosi mwaka huu kujiandaa na mchezo huo utakaochezwa kwenye uwanja wa Mandela, uliopo Namboole, Uganda, utakaofanyika Septemba 8 mwaka huu.

Wakati Uganda ikitangaza kikosi chake Kocha mpya wa Stars, Emmanuel Amunike, nyota wa zamani wa Nigeria, aliyemrithi Salum Mayanga, yeye bado hajatangaza kikosi chake.

Kocha wa Uganda, Sebastien Desabre, amemtaja Okwi ambaye ni mfungaji bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu uliopita akiwa na mabao 20.

Mbali ya Okwi pia beki wa Simba, Juuko Murushid na mlinzi wa Azam FC, Nico Wadada wameitwa kwenye kikosi hicho, lakini beki wa Singida United huku Shaffiq Batambuze akiachwa.

Katika kikosi hicho cha Uganda kwa ajili ya kuikabili Stars kimewajumuisha wachezaji 18 wanaocheza soka la kulipwa ikiwemo Ulaya huku wachezaji 12 wakitokea timu zinazocheza Ligi ya nyumbani.

Walioitwa ni Dennis Onyango, Jamal Salim, Charles Lukwago, Nicholas Sebwato, Denis Iguma, Nico Wadada, Godfrey Walusimbi, Isaac Muleme, Juuko Murshid, Denis Awany, Isaac Isinde, Musitafa Mujuzi, Hassan Wasswa, Khalid Aucho, Ibrahim Sadam, Tadeo Lwanga na Yasser Mugerwa.

Wengine ni Luwagga Kizito, Joseph Ochaya, Moses Opondo, Allan Kateregga, Faruku Miya, Moses Waiswa Martin Kizza, Okwi na Yunus Sentamu.

Chanzo: mwananchi.co.tz