Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

‘Nzi’ wawakera wachezaji wa England

9565 Nzi+pic TZWeb

Wed, 20 Jun 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Wadudu waliozagaa uwanjani wakati wa mechi ya England dhidi ya Tunia jana Jumatatu usiku, waligeuka karaha kwa wachezaji uwanjani hapo baada ya kuwazingira usoni.

Wadudu hao walionekana kwenye kamera za runginga wakimzingira nyota wa Manchester City, Raheem Sterling kwenye dimba la Volgograd Arena.

Nyota wengine wa England, Jesse Lingard na Danny Welbeck walionekana kukerwa na wadudu hao waliokuwa wamesambaa uwanjani.

Wadudu hao walionekana pia wakiingia masikioni, hivyo kuwafanya baadhi ya wachezaji wakati mwingine kuziba masikio na pua.

Licha ya kero hiyo ya wadudu, kikosi cha England kiliibukana na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Tunia mabao yaliyowekwa wavuni na Hary Kane.

Chanzo: mwananchi.co.tz