Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nyuma ya pazia namba za ajabu za jezi za wanasoka duniani

Jezi Pic Data Nyuma ya pazia namba za ajabu za jezi za wanasoka duniani

Wed, 3 Feb 2021 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

ISTANBUL, UTURUKI. MAMBO ya kushangaza yanayomhusu fundi wa mpira Mesut Ozil kwa sasa ni uchaguzi wa namba ya jezi yake baada ya kutua Fenerbahce.

Kiungo huyo mchezeshaji aliamua kuachana na Arsenal na kwenda kujiunga n miamba hiyo ya Uturuki na kuchagua kuvaa jezi yenye namba 67.

Bila ya shaka kitu ambacho Ozil alitaka ni kuondoka kwenye jinamizi la kukaa tu benchi kwenye kikosi cha Arsenal baada ya Kocha Mikel Arteta kumwondoa kwenye vikosi vyake vyote vya msimu huu.

Hata hivyo, namba hiyo mpya ya jezi aliyochagua huko kwenye timu yake ya Fenerbahce ina sababu maalumu.

Namba za jezi za wachezaji zinaripotiwa zote zimekuwa na sababu maalumu, wengine wanachagua kwa mambo ya kishirikina na wengine ni umaarufu tu kama ilivyo jezi Namba 7 kwenye kikosi cha Manchester United.

Ozil si mchezaji wa kwanza kuchagua jezi yenye namba ya ajabu kutokana na sababu mbalimbali. Hawa hapa mastaa wengine waliowahi kushangaza wengi kutokana na namba za jezi walizochagua kuzivaa kwenye timu zao mpya.

Chanzo: mwanaspoti.co.tz