Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nyuki wasimamisha mechi Yanga na Iringa United

89503 Pic+nyuki Nyuki wasimamisha mechi Yanga na Iringa United

Sat, 21 Dec 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

HALI ilikuwa si hali  ndani ya Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam katika mchezo kati ya Yanga na Iringa United wa Kombe la Shirikisho baada ya kundi kubwa la nyuki kuvamia uwanjani hivyo  kuleta taharuki kwa wachezaji, wamauzi na mashabiki.

Kundi hilo la nyuki lilipita uwanjani  dakika ya 53 na kuwafanya wachezaji wa timu zote mbili pamoja na wamauzi kulala chini.

Baada ya wachezaji kulala, beki wa Yanga Ali Mtoni Sonso alionekana kunyanyuka ghafla huku akijikung'uta kichwani akiashiria kung'atwa na  wadudu hao hivyo kukimbia nje kwenye benchi la timu yao ili kpata huduma ya kwanza.

Nyuki hao hawakuishia uwanjani tu kwani walienda mpaka katika baadhi ya majukwaa na kusababisha mashabiki kulala chini na wengine kukimbia kujiokoa.

Tukio hilo lilidumu kwa dakika sita na dakika ya 59  mwamuzi aliashiria mchezo kuendelea baada ya hali kuwa sawa na nyuki hao kutokomea.

Chanzo: mwananchi.co.tz