Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nyota wanne Mwadui kuikosa Simba, Kocha wala hana presha

Mwadui Pic1 Data Nyota wanne Mwadui kuikosa Simba, Kocha wala hana presha

Sun, 18 Apr 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Shinyanga. Wakati Mwadui ikiendelea kujiandaa na mchezo wake wa leo dhidi ya Simba, timu hiyo itawakosa nyota wake wanne akiwamo Nahodha na beki kisiki, Joram Mgeveke ambaye anatumikia adhabu ya klabu hiyo.

Mwadui ambao wanahaha kujinasua mkiani, leo Jumapili watakuwa nyumbani kwenye uwanja wa CCM Kambarage kuwakaribisha Simba ambao tayari wameshatua mjini hapa tangu usiku.

Mwanaspoti imefahamishwa kuwa Mgeveke ambaye ndiye mkongwe kikosini humo ataukosa mpambano wa leo kutokana na adhabu aliyonayo ambayo haijajulikaba itakoma muda gani.

Imeelezwa kuwa Beki alilimwa barua na mabosi wa timu hiyo kwa madai ya kuendesha mgomo tangu timu hiyo ilipokuwa ikijiandaa na mchezo wao na Mbeya City zaidi ya wiki mbili zilizopita.

Mgeveke ambaye aliwahi kukipiga kwa Wekundu, imeelezwa kuwa viongozi walimpa barua ya kumsimamisha kwa kile walichodai kuwa ameshawishi wenzake kugoma kutokana na madai yao ya mshahara.

Mwanaspoti imemsaka Mgeveke ambaye amekiri kuwa nje ya timu, huku akibainisha kuwa adhabu hiyo ni uonevu kwani hajawahi kushiriki au kushawishi kitu hicho kambini.

Related Balaa la Kagere, Chama si mchezo"Hata mechi ya JKT Tanzania sikuwepo nimesimamishwa wakidai nilishawishi mgomo kwahiyo hata mechi ya Simba sitakuwapo japokuwa nawaombea mema kwani tukipoteza mchezo huo hali itakuwa mbaya zaidi" amesema Mgeveke.

Pia wengine ambao hadi sasa imeelezwa kuwa hawajawasili kambini ni Kipa Mohamoud, Ismail Ally na Emanuel Memba ambao tangu wapewe likizo fupi kipindi cha maombolezo ya kifo cha aliyekuwa Rais, John Magufuli hawajarejea tena.

Hata hivyo Kocha wa timu, hiyo Salhina Mjengwa amesema kutokuwapo kwa nyota hao inaweza au isiweze kubaribu mipango yao ya kuchukua pointi tatu leo.

"Ni kweli kuna wachezaji kama sita hawapo kwa sababu mbalimbali lakini timu haiwezi kutegemea mtu mmoja, tunaandaa kikosi kulingana na mchezo husika hivyo hata kipindi wapo bado tulifungwa" amesema Mjengwa.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz