Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nyota wanaotarijiwa kung'ara Simba day leo

70222 Nyota+day

Wed, 7 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

SIMBA Day inaingia msimu wa 11 tangu iasisiwe mwaka 2009 chini ya uongozi wa akina Hassan Dalali na leo kuna shughuli kubwa inasubiriwa kufanyika kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

Kwa wiki nzima Simba imekuwa ikifanya shughuli mbalimbali za kijamii na jana walikuwa Bunju kuweka jiwe la msingi la uwanja wao, lakini utamu utakuwa leo Jumanne wakati wa mechi ya kilele cha Simba Day dhidi ya Power Dynamo ya Zambia.

Mashabiki wa soka wanatarajia kufurika uwanjani kama kawaida ili kushuhudia utambulisho wa nyota wapya na kuna baadhi huenda wakafunika kwenye tamasha hilo

Baadhi ya nyota wanaotabiriwa kung’ara kwenye utambulisho ni pamoja na Ibrahim Ajibu, ambaye amerejeshwa Msimbazi kutoka Jangwani alikokuwa akiichezea Yanga kwa misimu miwili.

Pia kuna Beno Kakolanya ambaye Yanga ilikuwa inamhitaji kwa hali na mali, lakini jamaa akaamua kuwakaushia na kukimbia Msimbazi na mashabiki wa Simba watatumia kama fimbo ya kutaka kuonyesha namna wanavyokubali uwezo wake na kuinyamazisha Yanga.

Kadhalika kuna Gadiel Michael mmoja kati ya mastaa waliowapasua vichwa mabosi wa Yanga waliokuwa wakipambana kumbakisha naye kuwazuga hadi alipiotoka Misri kwenye Afcon 2019 na kutambulishwa kuwa ni mali ya Simba.

Pia Soma

Mashabiki wa Wekundu wa Msimbazi watalitumia hilo kama fimbo ya kuwachapia Yanga kuonyesha kwamba timu yao ina pesa, ndio maana wamechukua mchezaji yeyote wanayemhitaji na hilo litamfanya Gadiel aonekane shujaa Taifa.

Mkali mwingine ambaye atatikisa Taifa huenda akwa ni MK14, Meddie Kagere ambaye mashabiki wa Yanga hawana hamu naye kwa namna alivyowatibulia ubingwa msimu uliopita kwa bao lake lililowazima Uwanja wa Taifa.

Mabao yake 23 yaliyompa Tuzo ya Mfungaji Bora yamekuwa yakimfanya Kagere kuwa mmoja ya nyota wanaopendwa na kutajwa zaidi na mashabiki wa Simba, na leo ni ngumu kumkaushia hata kama Simba Day hii kwake ni ya pili.

Mkali mwingine ambaye mashabiki wana hamu naye ni kiungo Msudani, Shoboub Sharaf Eldin ambaye mashabiki wa Yanga wamekuwa wakimponda, lakini Simba wameukubali mziki wake katika mechi alizocheza kambini Afrika Kusini kama ambavyo pia itakuwa kwa Wabrazili watatu waliosajiliwa yaani Tairone da Silva, Gerson Vieira na Wilker Da Silva.

Chanzo: mwananchi.co.tz