Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nyota wa raga ya wachezaji saba Kenya Collins Injera astaafu

Nyota Wa Raga Ya Wachezaji Saba Kenya Collins Injera Astaafu Nyota wa raga ya wachezaji saba Kenya Collins Injera astaafu

Tue, 24 Jan 2023 Chanzo: Bbc

Collins Injera, mmoja wa wachezaji nyota wa Kenya wanaocheza raga ya wachezaji saba, ametangaza kustaafu kutoka mchezo huo.

Anavipumzisha viatu vyake kama mfungaji bora wa pili duniani katika sekunde saba baada ya kuvuka mstari mara 279.

Katika kipindi chote cha miaka 17 ya kucheza raga ya kimataifa, Injera alikuwa mtu muhimu katika kikosi cha saba cha Kenya huku pia akiwakilisha kikosi cha wachezaji 15.

"Kila kitu lazima kifikie mwisho, wakati mwingine," Injera alisema.

"Siku zote nimesema kwamba nitajua ni wakati, kwa sababu mwili wangu utaniambia."

"Kwa miezi michache iliyopita 'umenizungumza' sana, mwishowe, nimeamua kuusikiliza," alisema.

"Natumai nimewaletea ninyi nyote fahari."

Injera alikuwa sehemu ya kikosi cha Simbas katika michuano mitano iliyopita ya Rugby Sevens, na kufika nusu fainali mwaka 2009 na 2013 - ingawa nia ya kuwa nao kwenye Kombe la Dunia la raga imeishia kwa mafadhaiko.

Mojawapo ya mambo muhimu katika maisha ya Injera ni kushinda mkondo wa Singapore wa Msururu wa Saba Duniani mwaka wa 2016, alipofunga majaribio mawili na kutajwa kuwa mchezaji bora wa fainali walipoifunga Fiji 30-7. Pia aliwakilisha Kenya kwenye Michezo ya Olimpiki ya 2020 jijini Tokyo.

Chanzo: Bbc