Mwanariadha anayeshikilia rekodi za dunia katika mbio za mita 100 na mita 200, Usain Bolt kutoka Jamaica anaripotiwa kupoteza mabilioni ya pesa kupitia ulaghai mkubwa.
Kulingana na jarida la AFP, mamlaka inayosimamia fedha nchini Jamaica imeanzisha uchunguzi dhidi ya kampuni ya kuwekeza pesa ambayo Bolt alikuwa amewekeza pesa zake na ambazo zimeofiwa kutoweka kwa njia za ulaghai.
Meneja wa Bolt Nugent Walker aliliambia gazeti la Jamaica Gleaner kwamba mwanariadha huyo aliyestaafu, amekuwa na uwekezaji na kampuni hiyo kwa zaidi ya muongo mmoja.
"Hatua zote muhimu zimechukuliwa ili kufafanua jambo hili.” Walker aliambia jarida hilo, akisema mwanariadha huyo aligundua hitilafu kwenye akaunti yake siku ya Jumatano.
Kwa mujibu wa taarifa toka kwenye mitandao ya nchini Jamaica ukiwemo Jamaica Observer, umeripoti kwamba Bolt amepoteza kiasi cha ($10 million) zaidi ya TSh. Bilioni 23. Kwa sasa akaunti yake inasoma ($2,000) takribani TSh. Milioni 4