Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nyota Simba wapagawa kwa ufundi wa Mbelgiji

9371 Pic+simba TanzaniaWeb

Thu, 2 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Patrick Aussems ameanza kuonyesha vitu vya uhakika timu hiyo inapojiandaa kwa ajili ya msimu mpya wa Ligi. Simba imeweka kambi ya wiki mbili nchini Uturuki kwa lengo la kujiweka sawa kwa ajili ya kutetea ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2018/19 itakay-oanza Agosti 18, pamoja na Ligi ya Mabingwa Afrika.

Katika kile kinachoonekana kuwa ni kudhamiria kufanya kweli kwenye mashindano hayo ya Afrika, Mbelgiji huyo aliyejiunga na Simba muda mfupi kabla ya safari ya kuelekea Uturuki sasa ndio ameanza kuonye-sha vitu vya uhakika.Aussems aliyeanza kazi kwa kuwapa vijana wake mazoezi ya utimamu wa mwili ‘body fitness’ sasa ameg-eukia kwenye ufundi ‘staminal’ akiwapa wachezaji wake wote fursa kwa kila mmoja kuonyesha ufundi wake na kulithibitishia benchi la ufundi kuwa anastahili kuwepo kwenye kikosi cha kwanza.Achana na kumwagiwa sifa na wasaidizi wake, lakini hata wache-zaji wameonekana kukunwa na hilo na wote wameonyesha matumaini ya kupata mafanikio chini yake. Baadhi ya wachezaji waliliambia Mwananchi kwa namna Kocha ana-vyowashirikisha kila mmoja ni wazi kuwa timu itafanya makubwa kwa sababu wote lao ni moja na hakuna atakayekuwa na kinyongo.

Mshambuliaji mpya wa Simba, Mohammed Rashid, aliyesajiliwa hivi karibuni akitokea Tanzania Prisons ya Mbeya, alisema hakutarajia kumpata Kocha wa aina ya Aussems kwani amewafanya wachezaji wote kujiona sawa baada ya kuwahamasisha wote kumthibitishia uwezo.

“Kwa kweli Kocha wote tumemkubali kwa sababu kitu cha kwanza alichokifanya ametukalisha na kutueleza kilichomleta Simba na sababu ya sisi kusajiliwa, ametu-ambia kile anachokitaka sisi tushirikiane naye kukifanya ambacho ni kuandika historia ili hata tukiondoka Simba tubaki tukikumbukwa milele katika historia ya Klabu hiyo,” alisema na kuongeza. “Kocha amekataa uvivu na uzembe ameweka wazi kuwa anapenda kumuona kila mmoja wetu akijituma, baada ya kuzungumza kwa pamoja, amekuwa pia akiketi na mchezaji mmoja mmoja na kuzungumza naye huku akimuhoji na kumuelekeza kile anachopaswa kukifan-ya.”

Alisema wamebaini kuwa kila mchezaji atakuwa na nafasi kwenye kikosi iwapo atajituma na kufuata maele-kezo ya Aussems. Rashid alisema chini ya Aussems anaamini Simba itafanya makubwa msimu huu kwani kila mchezaji sasa amejiapiza kuitumikia timu hiyo kwa uwezo wake wote na lengo ni kuitekeleza ahadi ya kocha huyo ya kutwaa mataji.

Chanzo: mwananchi.co.tz