Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nyota Simba wajipa matumaini

Matumaini Pic Data Nyota Simba wajipa matumaini

Thu, 20 May 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

IKIWA imesalia siku moja wekundu wa Msimbazi Simba kutaka kuweka historia ya aina yake katika uwanja wa Benjamin Mkapa, nyota wa timu hiyo wamepania kupambana kufa na kupona kupata matokeo.

Simba jana ilitoa ruhusa ya kufanya mahojiano na wachezaji na kocha wa timu hiyo huku leo na kesho wakipiga marufuku kuudhuria mazoezi yao kwa kuwa benchi la ufundi liko bize na maandalizi ya mchezo huo.

Simba ilikumbana na kichapo cha mbwa mwizi katika mchezo wa awali wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kukubali kichapo cha mabao 4-0 kutoka kwa Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini hivyo ili aweze kusonga mbeke anatakiwa kushinda mabao 5-0.

Nahodha wa kikosi hicho John Bocco amesema, wao kama wachezaji watahakikisha wanapambana kupata matokeo katika mchezo huo ili waweze kutimiza malengo.

Amesema, mchezo huo watapigana kadri ya uwezo wao wapate matokeo akiamini lolote linaweza kutokea katika mchezo huo muhimu kwao.

"Kila timu inahitaji matokeo katika mchezo huo, na sisi kama wachezaji ni jukumu letu kuhakikisha tunapambana kupata matokeo katika mchezo huo ambayo yatazidi kutuweka katika sehemu nzuri maana tukipoteza huo mchezo ndio tumeondolewa, katika kutimiza malengo,"amesema Bocco.

Kwa upande wake Erasto Nyon anasema, matokeo yaliyopita yaliwaumiza sana, lakini ndio mpira kwani hata wao wachezaji hawakutegemea kilichotokea.

"Tutahakikisha tunapambana kupata matokeo ambayo yatatufanya kutimiza malengo tuliyoyapanga toka mwanza mwa michuano hii, wanasimba waendelee kutusapoti sisi wachezaji tutahakikisha tunapambana kupata matokeo," amesema.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz