Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nyoso amuweka mfukoni Kagere

56778 Pic+kagere

Mon, 13 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Beki nguli wa Kagera Sugar, Juma Said ‘Nyoso’ jana alifanya kazi ya ziada kulinda vyema lango la timu yake ya Kagera Sugar, baada ya kumdhibiti mshambuliaji nyota wa Simba, Meddie Kagere.

Nyoso ambaye ni beki mkongwe nchini, alicheza kwa kiwango bora mchezo wa jana ambao Kagera ilishinda bao 1-0 kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Beki huyo wa zamani wa Ashanti United, Simba na Taifa Stars alimpa ulinzi mkali Kagere ambaye alikuwa akihaha kusaka mabao katika mchezo huo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Kagere ambaye anaongoza kwa kufunga mabao 20 kwenye ligi hiyo, hakufua dafu mbele ya Nyoso kwa kuwa mipango yake iliharibiwa kila mara alipokuwa akitaka kumuona kipa wa Kagera, Said Kipao.

Nyoso aliyecheza beki wa kati akishirikiana na Juma Shemvuni walitoa ulinzi pia kwa Emmanuel Okwi ambaye aliyekuwa akisaka kwa nguvu mabao. Simba imeendeleza uteja kwa Kagera kwani msimu uliopita licha ya kutwaa ubingwa ilifungwa mechi moja tu dhidi ya Kagera kwenye Uwanja wa Taifa lilifungwa na Edward Cristopher.

Simba na Kagera Sugar zimevaana mara mbili msimu huu na katika mechi ya kwanza Simba ilichapwa mabao 2-1, kwenye Uwanj wa Kaitaba, Bukuba.

Pia Soma

Pambano lilivyokuwa

Dakika 17 kiungo wa Simba, Mohammed Ibrahim alimuwekea pasi Okwi lakini alipiga shuti juu. Kagere aliyekuwa akipokea mipira mingi iliyotokea pembeni huku akiwa kati kati alishindwa kufunga mara kadhaa licha ya kuingia ndani ya eneo la hatari la Kagera.

Okwi aliyekuwa akishuka katika eneo la kiungo la Simba kupokea mipira ya akina Mzamiru Yassin, James Kotei, Hassani Dilunga na Ibrahim kama ilivyokuwa kwa Kagere alishindwa kufunga. Dakika ya 39 beki wa kushoto aliyekuwa nahodha katika mechi ya jana Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ alimtengea pasi Hassan Dilunga, ambaye alipiga shuti lililopanguliwa na kipa wa Kagera.

Dakika ya 41 Kagere Sugar ilifanya shambulizi baada ya krosi iliyopigwa beki David Luhende kumbambatiza Tshabalala aliyejifunga alipotaka kukontroo mpira huku kipa Aishi Manula akiwa amejiandaa kudaka.

Tukio hilo lilimkasirisha Manula ambaye alionekana akimtolea maneno makali beki huyo. Dakika 46 Chama aliingia kwa kasi baada ya kumuwekea Kagere pasi nzuri ndani ya boksi lakini alipiga kiki juu.

Simba walipata dakika 79, iliyokwenda kupigwa na Chama aliyomkuta Rashid Juma akuwa mwenyewe na kupiga kichwa ambacho kilinyakwa na kipa Said Kipao. kumlizika mwamuzi wa akiba Liston Hiyari aliongeza dakika saba, dakika hizo za nyongeza Kagera walimtoa Ramadhani Kapera na kuingia Amad Waziri.

Kikosi Simba: Aish Manula, Zana Coulibaly, Mohammed Hussein, Yusuf Mlipili, Erasto Nyoni, James Kotei, Hassan Dilunga, Mzamiru Yassin, Meddie Kagere, Emmanuel Okwi na Mohamed Ibrahim.

Kikosi Kagera Sugar: Said Kipao, Mwaita Gereza, David Luhende, Juma Nyosso, Juma Shemvuni, Peter Mwalyanzi, Kassim Hamisi, Ally Ramadhan, Ramadhan Kapera, Paul Ngalyoma na Evans Ludovic.

Chanzo: mwananchi.co.tz