Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nyoni afichua siri ya ushindi

Nyoni Picha Data Nyoni afichua siri ya ushindi

Tue, 22 Jun 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

By Daudi Elibahati

BEKI kisiki wa Simba Erasto Edward Nyoni ameweka wazi sababu kubwa ya timu hiyo kuendelea kufanya vizuri katika michuano mbalimbali.

Nyoni ambaye amekuwa tegemeo kikosini hapo licha kuwa na ushindani katika nafasi anayocheza, alianza kuitumikia Simba toka mwaka 2017 akitokea Azam FC, amesema kuwa sababu kubwa ya timu hiyo kufanya vizuri ni kutokana na wachezaji kucheza kwa ajili ya kuipigania timu na sio kwa maslahi ya mtu binafsi.

"Wachezaji wanajitambua wanajua timu inataka nini? viongozi, mashabiki pia wanajua malengo ya klabu ni kuendelea kuwa juu zaidi ya hapa tulipo kwa sasa, hali inayotufanya kujituma na kupigana kwa ajili ya nembo ya klabu" amesema Nyoni.

Aidha ameongeza kuwa sababu nyingine ya timu hiyo kufanya vizuri ni kutokana na ushindani mkubwa uliopo kikosini hali inayomfanya kila mchezaji kujituma kwa kupigania namba ili aweze kupata nafasi ya kucheza mara kwa mara.

"Kama unavyojua Simba imekuwa na maingizo mengi ya wachezaji bora kila msimu katika kikosi chetu, hali inayofanya kwa kiasi kikubwa ushindani kuongezeka na kuwa mkubwa kwetu" amesema

katika hatua nyingine nyota huyo alisema kuwa kuwepo kwa Umoja na mshikamano kati ya wachezaji na viongozi ni sabubu nyingine inayowatofautisha na timu nyingine.

"Viongozi wanajua umuhimu wetu, hali hii ya kutujali kama wachezaji inatufanya kupigania sana timu yetu kwa ajili ya mashabiki zetu ambao daima wamekuwa wakitupa sapoti kila kukicha" amesema.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz