Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nyoni, Manula, Dilunga wawashusha presha mashabiki

12926 Pic+simba TanzaniaWeb

Tue, 21 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mwanza. Nyota wa Simba wamewatuliza mashabiki wa klabu hiyo na kuwaambia kuwa wako fiti kinoma kwenye Ligi Kuu itakayoanza Jumatano.

Simba itaanza kutetea taji lake kwa kuivaa Prison katika mchezo utakaopigwa Jumatano kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.

Wakizungumza mtandao wa Mwanaspoti, wachezaji wa Simba, Erasto Nyoni, Aishi Manula na Hassan Dilunga walisema wako fiti hivyo mashabiki wategemea mambo makubwa kutoka kwao kwenye Ligi Kuu itakayoanza Jumatano ya Wiki hii.

Nyoni alisema kwa mazoezi ya nguvu waliyofanya  katika kambi yao ya Uturuki yamewaweka vizuri jambo ambalo amesema kwa sasa wako tayari kwa Ligi Kuu.

“Tumejipanga kwa kweli kuhakikisha tunatetea ubingwa wetu hivyo mashabiki wasiwe na presha waje kwa wingi kila mechi tutakayocheza hatutowaangusha”alisema Nyoni.

Kipa Manula alisema kikosi chao kimekuwa imara kwani wamejifua vya kutosha hivyo mashabiki wa timu hiyo wategemee ushindi kwa kila mechi wanayocheza.

“Najua Ligi itakuwa na ushindani mkubwa, lakini tutapambana kila mchezo ili tuweze kupata matokeo mazuri ambayo yatatusaidia kuweza kutetea ubingwa wetu,”alisema Manula.

Naye Dilunga alisema wamejiandaa vya kutosha kutetea ubingwa wa Ligi Kuu ambapo amesema wataanza ligi kwa kuitandika Prison katika mchezo wa keshokutwa.

Chanzo: mwananchi.co.tz