Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nyika atua Kigali, afurahia morali

14504 PIC+NYIKA TanzaniaWeb

Wed, 29 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Rweanda. Mwenyekiti wa kamati ya mashindano wa Yanga Hussein Nyika amewasili hapa Kigali leo Jumatano.

Nyika amefika kuongeza nguvu kwa timu yake inayoshuka uwanjani mchana kucheza na Rayon Sport.

Mara baada ya kufika Nyika amesema amefurahishwa na utulivu wa kambi yao.

Amesema mbali na utulivu amekutana na makocha na wachezaji na kwamba morali yao iko huu.

Naye Hamad Islam amesema Watanzani wanatakiwa kuiombea dua Yanga na kwamba maandalizi yao yako sawa.

Wawakikilishi hao wa Tanzania kwenye Kombe la Shirikisho Afrika, Yanga ilitua salama hapa Kigali, nchini Rwanda na hoteli waliyofikia ina rekodi nzuri kwao kwa kupata ushindi mkubwa dhidi ya timu za hapa.

Yanga iliyotua katika jiji la Kigali, imeweka kambi katika Hoteli ya Mirror iliyopo umbali mfupi kutoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kigali.

Awali, kabla ya kufikia hapo Yanga ilificha hoteli ambayo itafikia jambo ambalo liliwakera mabosi wa Chama cha Soka Rwanda (Ferwafa) walioweka wazi kuchukizwa na ukimya huo.

Baada ya kuwasili, Yanga ilionekana kujiandalia usafiri na kufikia Hoteli ya Mirror ambayo waliitumia misimu miwili iliyopita.

Chanzo: mwananchi.co.tz