Rais wa Chama cha Mpira wa Miguu Malawi (FAM), Walter Nyamilandu amechaguliwa kuwa mjumbe wa Baraza la Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) akiwakilisha nchi za Afrika zinazozungumza lugha ya Kiingereza.
Nyamilandu ameshinda nafasi hiyo baada ya kupata kura 35 huku akimpiku Rais wa Chama cha Soka Afrika Kusini (SAFA), Danny Jordaan aliyepata kura 18.
Uchaguzi huo umefanyika leo jijini Sharm El Sheikh huko Misri ambako kunafanyika mkutano wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF).
Aliyekuwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) alikuwa ni miongoni mwa wagombea watatu wa nafasi hiyo lakini aliangika baada ya kupata kura 14.
Uchaguzi huo ulilazimika kurudiwa baada ya Nyamilandu aliyeongoza mwanzoni kupata kura 23 ambazo hazikuvuka idadi ya zaidi ya nusu ya kura zote 53