Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Niyonzima afunguka kilichomrejesha Yanga

HARUNA.webp Niyonzima afunguka kilichomrejesha Yanga

Thu, 30 Apr 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

KIUNGO wa kimataifa wa Yanga, Haruna Niyonzima, amesema Tanzania ni mahali pazuri kwake ndio sababu kubwa ya kukubali kurejea kucheza hapa nchini kwa mara ya tatu.

Hata hivyo Niyonzima alisema amekubali kurejea kwa mara ya pili ndani ya kikosi cha Yanga bila ya kuweka mbele maslahi binafsi.

Niyonzima alisema pia licha ya Yanga kuonekana haina wakati mzuri, bado alikubali kujiunga nayo kwa sababu kwake aliangalia mambo mengi hadi kufikia uamuzi wa kusaini mkataba mwingine na klabu hiyo.

"Nimerudi Yanga kwa sababu ndio timu ninayoiheshimu na ni timu ninayoifurahia, ni kweli tunaangalia maslahi, lakini lazima uwe na sababu zako binafsi, kwa hisia zangu binafsi ndio zilipelekea kukubali kurejea," Niyonzima alisema.

Kiungo na nahodha huyo wa Timu ya Taifa ya Rwanda (Amavubi), alisema aliondoka Yanga bila ya kuwa na tatizo lolote na ilitokana na mipango ya Mwenyezi Mungu.

"Hata nilipoenda Simba, watu walitegemea kupata vitu vikubwa kutoka kwangu, lakini haikuwa hivyo, ni mipango ya Mwenyezi Mungu, siwezi kusema sana,"

Mnyarwabnda huyo aliongeza majeruhi aliyopata ni moja ya sababu zilizopelekea ashindwe kuonyesha kiwango chake kilichozoeleka.

"Naweza kusema haikuwa bahati yangu pale, kila mchezaji anatamani anapokwenda aonyeshe kiwango kizuri, lakini haikuwa hivyo, mimi nilipoondoka Yanga hakukuwa na tatizo, nilikuwa napewa mshahara wangu kama kawaida, hata kama ulikuwa unachelewa, Jumatatu haiwezi kufanana na Jumanne," Niyonzima alisema.

Aliongeza kikosi cha Yanga ni kizuri, lakini kinahitaji muda ili kuimarika na wachezaji kucheza kwa muda mrefu pamoja.

"Yanga tulichukua kikombe cha Ligi Kuu Bara mara tatu mfululizo, sio kama tulikuwa na kikosi hatari sana, lakini tulizoeana, mchezaji unajua ukipeleka mpira hapa, utamkuta mwenzako, huwezi kupata mafanikio haraka haraka," Niyonzima alisema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live