Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Niyonzima - Tutakomaa mpaka kieleweke

39705 Pic+niyonzima Niyonzima - Tutakomaa mpaka kieleweke

Mon, 4 Feb 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Kiungo wa Simba,Haruna Niyonzima amesema licha ya kwamba mchezo wao dhidi ya Al Ahly leo utakuwa mgumu lakini kama watapambana na kucheza kwa ushirikiano watapata matokeo mazuri. Simba itakuwa ugenini leo kuikabili Al Ahly  katika mchezo wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika utakaofanyika kwenye Uwanja wa Borg El Arab,mjini Alexandria Misri na utakaoanza saa 4:00 kwa saa za Afrika Mashariki. Niyonzima alisema licha ya hali ya hewa kuwa ya baridi kali lakini wameshazoea na kilichobaki ni kuingia uwanjani kupambana ili kupata matokeo mazuri. "Tunawashukuru viongozi kutuleta huku mapema kwani hali ya hewa sio nzuri nui baridi kali.Wakati tunafika ilitusumbua kidogo lakini kadri tulivyokaa tunazoea.   "Huu ni mchezo mkubwa na utakuwa mgumu lakini kama wachezaji tumejiandaa na tunajua nini kilichotuleta hapa.Naamini ushirikiano na kila mmoja akijituma basi tutapata matokeo mazuri"alisema Niyonzima

Chanzo: mwananchi.co.tz