Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Niyonzima, Juuko wajifua Simba

17852 Pic+niyo TanzaniaWeb

Wed, 19 Sep 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Nyota wa Simba, Haruna Niyonzima na Juuko Murshid wamejifua kwa mara ya kwanza katika kikosi cha mabingwa hao watetezi katika mazoezi yaliyofanya kwenye Uwanja wa Boko Veterans.

Niyonzima na Jjuuko wamejiunga na kikosi hicho baada ya kumaliza tofauti zao viongozi wa klabu hiyo.

Simba inajiandaa na mechi zake mbili za kanda ya ziwa dhidi ya Mbao na Mwadui ilifanya mazoezi chini ya makocha Patrick Aussems, Masoud Djuma na Adel Zrane.

Kocha Zrane alitumia muda mwingi na wachezaji Juuko na Niyonzima walioanza kwa kufanya mazoezi wenyewe kabla ya kujiunga na timu.

Katika mazoezi hayo kocha Zrane alikuwa na wachezaji walianza kikosi cha kwanza dhidi ya Ndanda wakati Aussems na Djuma waliwasimamia wachezaji walioingia kipindi cha pili sambamba na wale hawakusafili kabisa na timu.

Mazoezi wanayofanya ni kucheza mipira mingi kwa kupasiana pasi huku wakiwekwa katika makundi mawili.

Kundi moja limevaa bipsi na bluu na wengine njano na kila kundi likipasiana pindi wanapokuwa na mpira na ambao hawana wanasafa kusaka mpira huo.

Soma Zaidi : Masoud apigwa chini safari ya Simba Mwanza

Chanzo: mwananchi.co.tz