Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ninja awatuliza mashabiki Yanga

46254 Pic+ninja Beki wa Yanga Abdallah Shaibu

Fri, 6 Aug 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

BEKI wa Yanga, Abdallah Shaibu 'Ninja' amesema kupitia michuano ya Kombe la Kagame, ameendelea kuimarika, huku akiwataka mashabiki kutambua hayupo fiti asilimia 100 ndio anarejea kwenye mstari.

Ameliambia Mwanaspoti leo Ijumaa Agosti 6, 2021 kwamba kuna wakati mashabiki wanaweza wakamjia juu bila kujua lengo la kocha kumpa kucheza michuano hiyo.

"Kocha ametaka niendelee kuimalika kupitia michuano hii, nimesema mara nyingi kwamba siwezi kuanza kwa kasi wakati nilikaa kwa muda mrefu nje baada ya kuumia nikiwa na Prisons" amesema Ninja na kuongeza;

"Kupitia Kagame, mashabiki wawe bega kwa bega na wachezaji wasienza kuwalaumu, angali wanajua huu ni mwanzo wa kocha kukiandaa kikosi imara kwa ajili ya msimu ujao,"amesema.

Amesema mchezaji ni binadamu kuna wakati mwingine anaweza akaumizwa na maneno yao, jambo aliloshauri sio jema wakati wakuunganisha nguvu pamoja ili kuiandaa Yanga imara ya msimu unaokuja.

"Ni kweli mashabiki wanatamani kuona tunafunga kila mechi, lakini kuna wakati mchezaji ni binadamu yapo mambo mengi yanaweza yakamkuta, mfano mimi kuumia wakati nina shauku yakuifanyia kitu timu yangu, hivyo tushikamane,"amesema Ninja.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz