Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ngoma ngumu Watanzania Michuano ya Olimpiki

Felix Simbu Mwanariadha wa Tanzania,Felix Simbu

Sun, 8 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati michuano ya Olimpiki ikitazamiwa kufika tamati siku ya leo huko Tokyo, Japan kuna waliocheka na waliolia kwa washiriki linapokuja suala la kupeperusha bendera za nchi zao.

Hali imekua tete kwa Wanariadha watatu kutoka nchini Tanzania ,Felix Simbu,Gabriel Geay na Mwanadada Failuna Abdi Matanga ambao wameshamaliza ushiriki wao lakini wametoka mikono mitupu.

Failuna ambae alikimbia mbio kwa upande wa wanawake siku ya Jana alimaliza katika nafasi ya 24.

lakini Mapema leo siku ya Jumapili wanariadha wawili Felix Simbu na Gabriel Geay walishiriki katika mbio za Marathoni za kilometa 42.2 ambapo mshindi aliibuka Eliud Kpichonge raia wa Kenya akitetea medali yake ya dhahabu.

katika mbio hizo Mtanzania Felix Simbu alimaliza nafasi ya 7 huku mwenzake Gabriel Geay rekodi zikionesha hakufika hata nusu ya mbio hizo yaani kilometa 21.1.

"Tumemaliza mashindano salama,nimeingia kwenye top ten ya mbio hizi za olimpiki,nilidhamiria niweze kupambana ili nishinde medali lakini sijapata,kwa hiyo tunarudi nyumbani tuweze kujipanga kwa mashindano mengine kwa sababu haya yameshapita"amsema Simbu mara tu baada ya kumalizika kwa mbio hizo.

Simbu alitumia muda wa saa 2 dakika 11 na sekunde 35,wakati Kipchonge alitumia saa 2 dakika 8 na sekunde 38,nafasi ya pili ilikwenda kwa Mholanzi Nageeye alietumia saa 2:09:58 na nafasi ya tatu ilikwenda kwa Mbelgiji Abdi alietumia saa 2:10:00.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live