Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Neville awatuhumu wachezaji Man U

Gary Neville Neville awatuhumu wachezaji Man U

Tue, 19 Oct 2021 Chanzo: eatv.tv

Beki wa zamani wa Manchester United, Gary Neville amewatuhumu wachezaji wa klabu hiyo kwa kutoipambania timu na kufanya mambo kama watoto huku wakidhani wao ni bora kuliko ilivyokuwa enzi zao, wakati wanakubali kipigo cha bao 4-2 dhidi ya Leicester City Jumamosi.

Pia Neville amemsisitizia kocha Ole Gunnar Solskjaer kufanyia kazi madhaifu ya kikosi chake ikiwa ni pamoja na kuifanya timu kuwa na mshikamano ili kuondokana na mwenedo mbaya wa matokeo wanayoyapata uwanjani

Beki huyo wa zamani wa "Mashetani Wekundu" anasema kuwa haya sio matokeo ya kwanza ya kukatisha tamaa yaliyopatikana na timu ya Ole Gunnar Solskjaer kwani mpaka sasa tayari wamepoteza kwa Young Boys, Aston Villa na West Ham msimu huu.

Chanzo: eatv.tv