Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ndugai: Mafanikio ya Simba sihaba

444f64c51012bc3018d97f23b6f5df37.jpeg Ndugai: Mafanikio ya Simba sihaba

Tue, 25 May 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

SPIKA Job Ndugai amesema klabu ya Simba inapaswa kupongezwa kwa hatua iliyofikia ya kucheza robo fainali ya Ligi ya Mabingwa wa Afrika, kwani sihaba.

Ndugai aliyasema hayo bungeni mara baada ya kumalizika kwa kipindi cha maswali na majibu jijini hapa jana.

Alisema Simba kufika hatua ya robo fainali ya Michuano ya Ligi ya Mabingwa wa Afrika ni hatua ya juu.

“Kama Bunge ni lazima tupongeze kwa timu yetu ya Simba Sports Club kututoa kimasomaso kuweza kufika robo fainali ya Ligi ya Mabingwa wa Afrika, si padogo, si haba.”

“ Naona rafiki zetu (Yanga) nao wajitahidi badala ya ligi ya hapa hapa tuu wajitahidi kidogo waige, wasiogope, tunategemea mwakani.”

Aidha, Ndugai alipeleka pongeza kwa timu ya Namungo, ambayo imeshiriki kwa mara ya kwanza Michuano ya Kombe la Shirikisho la Afrika na kucheza hatua ya makundi.

“ Hata Namungo wamejitahidi ni mara ya kwanza wameingia kwenye mashindano makubwa wamejitahidi.”

“ Sasa wengine mpo wapi?, badala yake tunakuwa tunashangilia wageni tuu, jamani hiyo haipendezi hata kidogo. Lakini mwisho wa haya si tarehe 3 mwezi wa saba jamani, ndio majibu yatapatikana baada ya hapo tutakutana kwenye ukumbi huu tusikie mambo yakoje.”

“ Kwa kweli tunawapongeza TFF, Wizara na wote wanaohusika wakiwamo viongozi wa klabu, tumeiweka Tanzania kwenye ramani ya mpira.

Tutakubaliana kwamba wale wa Afrika Kusini Kaizer Chiefs wameendelea lakini yeyote aliyefuatilia mechi hizi mbili ataniambia klabu bora katika klabu zile ni ipi.”

Ndugai alisema kwa hatua ya soko iliopo, inaonesha Tanzania inaenda na kuwa itafika mbali kama nchi.

Chanzo: www.habarileo.co.tz