Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ndolanga, Wajumbe wamzungumzia Wambura kutoalikwa mkutano Mkuu TFF

39675 Kikao+tff+pict Ndolanga, Wajumbe wamzungumzia Wambura kutoalikwa mkutano Mkuu TFF

Mon, 4 Feb 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Arusha.Wakati aliyewahi kuwa makamu wa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Michael Wambura akilalamika kutoalikwa kwenye mkutano mkuu wa Shirikisho hilo unaofanyika Leo,  aliyekuwa rais wa FAT sasa TFF, Alhaji Mhidin Ndolanga na baadhi ya Wajumbe wa mkutano huo wamesema Wambura hana nafasi ya kuitwa kwenye mkutano huo.

Jana Wambura alilalamika kutopewa mualiko wa kuhudhuria mkutano huo ambao suala lake la kufungiwa maisha kutojihusisha linaweza kuibuka.

"Wambura alitaka aalikwe  kwenye mkutano kama nani, yeye alishafungiwa, alitaka mualiko wa nini," alihoji Ndolanga.

Alisema yeye Ndolanga ameudhulia mkutano huo kama Rais wa heshima wa Shirikisho, sanjari na wajumbe wengine kila mmoja kwa nafasi yake, sasa Wambura alitaka aalikwe kwa nafasi ipi.

Anachokifanya Wambura ni vurugu tu, ameshazoea," alisema Ndolanga.

Mjumbe wa mkutano mkuu, Ephraim Majinge wa Mwanza alisema ishu ya Wambura imefuata utaratibu hivyo hakustahili kuwepo katika mkutano huo sababu ameshafungiwa.

"Kama alishafungiwa alitarajia apewe mualiko wa nini? Alihoji Majinge nab kufafanua kwamba suala la kigogo huyo kutoalikwa ni sahihi.

Mjumbe mwingine, Emmanuel Chaula wa Katavi alisema ishu ya Wambura imekaa katika engo mbaya hivyo inampa ukakasi kuizungumzia.

Katibu Mkuu wa TFF, Wilfred Kidau alisema hawana mpango wa kumjibu Wambura kwa kile anachokifanya kwani alishahamua kwenda mahakamani.

" Alishakwenda Mahakamani, wacha ibaki hivyo, hatuna muda wa kumjadili mtu ambaye amekwenda nahakamani," alisema Kidau.

S:Wambura alifungiwa Machi mwaka Jana kutojihusisha na masuala ya Soka kutokana na makosa matatu ya kimaadili.



Chanzo: mwananchi.co.tz