Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ndege ya ATCL kuipeleka Stars Benin leo

95b10613931ea5202904b1ee5319bc81.jpeg Ndege ya ATCL kuipeleka Stars Benin leo

Fri, 8 Oct 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

TIMU ya soka ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, inatarajiwa kuondoka leo mchana kuelekea Cotonou, Benin kwa ndege ya Shirika la Ndege la ATCL.

Stars inatarajiwa kurudiana na Benin Jumapili wiki hii mchezo wa kuwania kufuzu Kombe la Dunia litakalofanyika mwakani nchini Qatar. Jana Stars ikiwa nyumbani Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam ilikubali kipigo cha bao 1-0 katika mchezo huo wa Kundi J.

Ofisa Habari wa TFF, Clifford Ndimbo amesema asubuhi hii kuwa maandalizi kwa ajili ya safari hiyo yamekamilika na timu itaondoka Dar es Salaam saa sita mchana.

Kutokana na kipigo cha jana, Stars sasa inashika nafasi ya tatu katika msimamo wa kundi hilo, ikibaki na pointi zake nne, huku Benin ikiongoza ikiwa na pointi saba na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) ni ya pili ikiwa na pointi tano. Madagascar inashika mkia na haina pointi.

Chanzo: www.habarileo.co.tz