Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ndege aliyeacha gumzo Kirumba

82258 Pic+kirumba Ndege aliyeacha gumzo Kirumba

Wed, 30 Oct 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mwanza. Wakati Yanga na Pyramids zikivaana katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika, moja ya tukio lililoibua mshangao ni ndege maarufu ‘Bwana Afya’ kukatiza ghafla katikati ya uwanja.

Ndege huyo alipita angani wakati mchezo ukiendelea na kuleta mshangao kwa wachezaji na mashabiki waliokwenda Uwanja wa CCM Kirumba.

Tukio hilo lilitokea kipindi cha pili ambapo ndege huyo alitokea upande wa kusini lilipokuwa lango la Yanga kwenda kaskazini kwa Pyramids.

Tukio hilo lilimpa hofu kipa nguli wa Pyramids, Ahmed Elshenawy aliyetaka kukimbia huku beki wake Abdallah Bakri akionyesha mshangao.

Yanga ilifungwa mabao 2-1 katika mchezo huo na timu hizo zitarudiana Novemba 3 nchini Misri.

Chanzo: mwananchi.co.tz