Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ndayiragije ataka nyota wanne tu Azam

63027 Pic+azam

Mon, 17 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Kocha Mkuu wa Azam FC, Etienne Ndayiragije anataka kusajili nyota wanne ili kuimalisha kikosi alichokikuta kabla ya msimu mpya haujaanza.

Ndaiyiragije amejiunga na Azam FC kwa mkataba wa miaka miwili akitokea KMC aliyoiongoza kumaliza nafasi ya nne katika Ligi Kuu Bara na kupata nafasi ya kushiriki Kombe la Shirikisho Afrika.

Mratibu Mkuu wa Azam FC, Philip Alando alisema kocha ameomba wasajili wachezaji wawili wa kimataifa na wawili wa ndani lengo ni kuhakikisha anaimarisha kikosi kwa msimu ujao.

"Amekaa na makocha waliokuwa wanakaimu nafasi ya Hans Van Pluijm kina Idd Cheche na ameridhishwa na wachezaji aliowakuta kikosini kikubwa alichosema anataka usajili wa nyota wanne tu."

"Mchakato wa kusaka nyota hao ameukabidhi kwa viongozi lengo ni kuandaa bajeti ambayo itakabidhiwa kwake kwa lengo la kufanya usajili wa nyota ambao anaamini wataweza kuonyesha uwezo ndani na nje ya nchi," alisema Alando.

Alando aliongeza kuwa kikosi cha timu hiyo kinatarajia kuingia kambini Juni 20 mwaka huu na kusisitiza kuwa mpango wao kwa kushiriki Kagame upo palepale wakiwa kama mabigwa watetezi.

Pia Soma

Chanzo: mwananchi.co.tz