Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nataka kushinda medali 6 mwaka 2022 - Kipchoge

Kipchoge 0 Mwanariadha Eliud Kipchoge

Fri, 18 Feb 2022 Chanzo: eatv.tv

Mwanariadha kutoka nchini Kenya Eliud Kipchoge ameweka dhamira ya kushinda mbio sita za marathon kwa mwaka 2022 huku akitarajiwa kushiriki kwenye mbio za marathoni za Tokyo nchini Japan mnamo march 6 .

Kipchoge, mwenye umri wa miaka 37, tayari ameshinda mara nne mbio za London Marathon, mbio za Berlin Marathon akishinda mara tatu huku zile za Chicago Marathon akishinda mara moja mnamo mwaka 2014 huku mwaka huu akitarajiwa kushiriki kwenye mbio za Tokyo, New York na Boston marathon.

“Malengo yangu yote nayatazamia kwenye mashindano ya Tokyo na nipo tayari kushindana, ni fahari kubwa kukimbia kwenye nchi ambayo ina utamaduni wa kipekee kwenye michezo tena nilishinda medali za dhahabu kwenye michezo ya olympiki iliyopita katika mji wa Sapporo " amesema Kipchoge

Eliud Kipchoge ambaye aliweka rekodi ya binadamu wa kwanza katika historia ya riadha ya kukimbia mbio za marathoni chini ya dakika mbili kwenye shindano lililojulikana kama INEOS 1:59 Challenge mjini Vienna nchini Austria mwaka 2019 japokuwa rekodi hiyo bado haitambuliki na shirikisho la kimataifa la riadhaa la IAAF.

Chanzo: eatv.tv