Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Naomi Osaka avuliwa Ubingwa wa US Open

59083328 303 Naomi Osaka avuliwa Ubingwa wa US Open

Sat, 4 Sep 2021 Chanzo: eatv.tv

Nyota namba tatu katika viwango vya ubora Duniani upande wa Wanawake, Naomi Osaka amesema atahitaji mapumziko kwa mara nyingine na hi ni baada ya kuvuliwa ubingwa wa mashindano ya US Open yanayoendelea kutimua vumbi nchini Marekani.

Osaka ameondoshwa mashindanoni katika mzunguko wa tatu wa mashindano hayo chipukizi mwennye umri wa miaka 18, Leylah Fernandez.

''Kwakweli sifahamu ni lini nitacheza tena ,nafikiri nahitaji kupata mapumziko ya kutosha ,kwasiku za hivi karibuni hata nikishinda sijisikii furaha, na hata nikipoteza najisikia vibaya, nadhani hali hii sio ya kawaida''alisema Osaka baada ya kupoteza mchezo.

Raia huyo wa Japan alijiamua kujiweka kando na hakushiriki katika michuano ya wazi ya Ufaransa(French Open) kwa maelezo kuwa alikuwa anapambana na matatizo ya afya ya akili tangu atwae grand slam yake ya kwanza mwaka 2018.

Vilevile hakushiriki katika mashindano ya Wimbledon kabla ya kurejea uwanjani katika Olimpiki yaliyofanyika nchini Japan mwaka huu.

''Kwakweli sifahamu ni lini nitacheza tena ,nafikiri nahitaji kupata mapumziko ya kutosha ,kwasiku za hivi karibuni hata nikishinda sijisikii furaha, na hata nikipoteza najisikia vibaya, nadhani hali hii sio ya kawaida''alisema Osaka baada ya kupoteza mchezo.

Chanzo: eatv.tv