Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Naomi Osaka atwaa ubingwa wa WTA Indian Wells

5019 Skysports Naomi Osaka Tennis 4259020 TZW

Tue, 20 Mar 2018 Chanzo: bongo5.com

Mwanadada raia wa Japani, Naomi Osaka kwa mara yake ya kwanza tangua kuanza mchezo wa tennis amefanikiwa kutwaa taji kubwa la michuano ya wazi la BNP Paribas au WTA Indian Wells baada ya kumshinda Daria Kasatkina.



 Mwanadada raia wa Japani, Naomi Osaka

Osaka amelitwaa taji hilo Jumapili hii kwa kumfunga Daria Kasatkina kwa jumla ya seti 6-3 6-2.



Mara baada ya ushindi huo, Osaka ameviambia vyombo vya habari kuwa lengo lake lilikuwa ni kutwaa taji hilo.

Naomi Osaka atinga fainali za Indian Wells kibabe baada ya kumtoa mchezaji namba moja kwa ubora duniani

Nilikuwa na hofu kubwa lakini nikajiamini na kusema malengo yangu ni kutwaa ubingwa.



Nilijua mpinzani wangu atapambana kwa kila pointi  hivyo siku na sababu ya kupoteza nilihakikisha nafanya vizuri na kufanya maamuzi yaliyo sahihi.

Chanzo: bongo5.com