Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nane kuwakilisha nchi mashindano ya pool table Sauzi

Pool Table Nane kuwakilisha nchi mashindano ya pool table Sauzi

Tue, 10 Oct 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Kikosi cha timu ya Taifa ya mchezo wa Pool Table wanaume kimekabidhiwa bendera ya Taifa na Ofisa Michezo wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT), Charles Mazungu kwa niaba ya Katibu Mkuu, Neema Misitha leo Oktoba 9 jijini Dar es Salaam.

Kikosi hicho kitakwenda jijini Johannesburg nchini Afrika ya Kusini kwa ajili ya mashindano ya All Africay Pool Association yatakayoanza Oktoba 11 hadi 16 mwaka huu.

Mazungu amewataka wachezaji hao kuhakikisha wanafanya vizuri katika mshindano hayo kwani wanakwenda kuwakilisha Taifa.

"Nyinyi ni wawakilishi wa watu milioni 60 zaidi tuliobaki nchini, mkifika mkawakilishe vyema Taifa licha ya kuwa mtakuwa wachezaji na mashabiki wachache watakaowashangilia, hilo lisiwavunje moyo"

Wachezaji watakaosafiri ni Charles Venance, Innocent Samwel, Jackson Stenphan, Abdalah Hussein, Festo Yohana, Norbert Kobelo, Amadeus Melkizedeck na Isaya Paulo, viongozi wawili na mashabiki saba.

Chanzo: Mwanaspoti