Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Namungo yaweka rekodi, 'yatingisha' Ligi Kuu Bara

NAMUNGO.jpeg Namungo yaweka rekodi, 'yatingisha' Ligi Kuu Bara

Fri, 26 Jun 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

SARE ya mabao 2-2 iliyopata Namungo FC dhidi ya Yanga kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam jumatano iliyopita, imefanya timu hiyo kucheza mechi 15 mfululizo za Ligi Kuu Bara bila kupoteza, ikiwa katika nafasi ya nne na pointi zake 55.

Namungo imeweka rekodi ya msimu, kwani hakuna timu yoyote kwenye Ligi Kuu ambayo imecheza idadi hiyo ya mechi bila kupoteza.

Simba inafuatiwa kwa kucheza mechi 12 mfululizo bila kupoteza, huku Yanga ikishika nafasi ya tatu kwa kuweka kucheza mechi 11 bila kupoteza msimu huu.

Kwa sasa hakuna timu itakayoweza kuweka tena rekodi hiyo, kwani kama Simba isipopoteza mechi yoyote itakuwa imecheza mechi 11 bila kupoteza na Yanga itakuwa imecheza mechi 12, kwa michezo yao ambayo imebakisha.

Mara ya mwisho kwa Namungo kupoteza mechi ilikuwa ni Januari 29, mwaka huu, ilipochapwa mabao 3-2 dhidi ya Simba na baada ya hapo imecheza mechi 15 bila kupoteza, ikishinda mechi tano na kutoa sare 10.

Namungo ilianza kuonyesha makali yake kwa kuinyuka Mbao FC mabao 3-0, kabla ya kutoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Alliance FC halagu ikatoka sare ya bila kufungana dhidi ya Ndanda, kabla ya kuichapa Singida United bao 1-0, baadaye ikalazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Mwadui FC.

Ilipata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya KMC, na kuichapa Azam bao 1-0, pia ikaisasambua Lipuli mabao 2-1.

Baada ya hapo ikaanza kutoa sare mfululizo ya bao 1-1 dhidi ya Mtibwa Sugar, bila kufungana dhidi ya Polisi Tanzania, sare ya bao 1-1 dhidi ya Biashara United na pia sare kama hiyo dhidi ya Yanga hiyo ikiwa ni mechi ya mzunguko wa kwanza na iliporejea baada ya mapumziko ya janga la corona ilianza kwa sare ya mabao 2-2 dhidi ya Coastal Union na kuichapa Kagera Sugar mabao 2-0.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live