Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Namungo yanasa mashine 2 Simba

68194 Namungo+pi

Thu, 25 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Namungo imenasa wachezaji 12 wapya wakiwemo wachezaji wawili wakitokea Simba, Mohammed Ibrahim ‘Mo’ na Paul Bukaba.

Pia klabu hiyo imewaondoa wachezaji 11 zikiwa zimebaki siku chache kabla ya dirisha la usajili kufungwa Julai 31, mwaka huu.

Akizungumza jana, Mwenyekiti wa Namungo, Hassan Zidadu alisema katika usajili huo kuna wachezaji saba wa kigeni.

Mbali na Ibrahim na Bukaba, wengine ni Carlos Protas (KMC), Paul Ngalema (Lipuli), George Makanga na Nurdin Barora (Biashara United) ambaye ni raia wa Bukina faso.

“Carlos Protas amesajiliwa kwa mkataba wa miaka miwili na wengine waliosalia wametia saini mwaka mmoja, tunaamini watasaidia kusukuma gurudumu la timu yetu,” alisema Zidadu.

Wachezaji wa kigeni ni Styve Nzigamasabo (Burundi) na Abdul Waheed Adesola-Lipuli (Nigeria), Stephen Duah (Ghana), Toure Sie Leopold (Ivory Coast), Sina Jerome (Congo) na Bigirimana Blaise (Burundi).

Pia Soma

Alisema wachezaji waliosajiliwa ni mapendekezo ya Kocha Hitimana Thierry. Pia aliyekuwa kocha msaidizi Bakari Malima ameondoka na nafasi yake imejazwa na Mganda Godefroid Okoko.

Mapema wiki hii, Namungo kutoka Ruangwa mkoani Lindi iliichapa Aigle Noir kutoka Burundi mabao 3-0 katika mchezo wa kirafiki uliochezwa Uwanja wa Azam Complex, Chamazi jijini Dar es Salaam.

Chanzo: mwananchi.co.tz