Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Namungo yakwama kupanda ndege tena

0ef64835536c9333ef3fa8f8f1ef5b6e.jpeg Namungo yakwama kupanda ndege tena

Mon, 24 May 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

NAMUNGO FC imekwama kupanda ndege tena kwa ajili ya mashindano ya kimataifa msimu ujao, baada ya kutolewa katika robo fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam kwa kichapo cha mabao 2-0 kutoka kwa Biashara ya Mara kwenye Uwanja wa Karume mjini Musoma jana.

Timu hiyo ya Lindi ambayo ilitolewa katika hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika hivi karibuni, ilishiriki mashindano hayo kwa mara ya kwanza kupitia mashindano hayo iliyotolewa baada ya kumaliza ya pili nyuma ya Simba Simba iliyotwaa ubingwa msimu uliopita.

Simba ilishiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa wa Afrika baada ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara na hivyo kuiachia Numungo iliyomaliza ya pili katika Kombe la Shirikisho kushiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Ushindi huo wa jana unaoifanya Biashara United kuwa timu ya kwanza kutinga hatua ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam msimu huu.

Biashara walipata bao la kwanza dakika ya tisa lililofungwa na Mpapi Nasibu na kuamsha morali ya timu hiyo kuliandama lango la wapinzani wao na kocha wa Namungo, Hemed Suleiman alilazimika kufanya mabadiliko ya kiufundi dakika ya 20 kwa kumtoa Ibrahim Abdallah ‘Imu Mkoko’ na kumuingiza Abeid Athuman.

Wenyeji waliongeza bao la pili katika dakika ya 39 kwa mkwaju wa penalti uliowekwa kimiani na mshambuliaji Kelvin Friday baada ya Deogratias Mafie kuchezewa faulo na Steven Duah, hadi dakika 45 zinatamalizika, Biashara ilikuwa mbele kwa mabao 2-0.

Chanzo: www.habarileo.co.tz