Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nahimana siyo wa mchezo mchezo hapo KMC

73231 Nahima+pic

Wed, 28 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Kipa wa KMC, Jonathan Nahimana amezidi kuonyesha uimara wa makipa katika kikosi chao pindi wanapokuwa wapo golini licha ya kupoteza michezo yao.

Katika mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu dhidi ya Azam Fc, Jonathan Nahimana alionyesha umahili wake katika kuokoa michomo ya wapinzani wake.

Nahimana alikuwa akiwapanga vizuri mabeki wake Abdallah Mfuko na Yusuph Ndikumana na kuwafanya washambuliaji wa Azam, Obrey Chirwa na Richard Djodi kushindwa kutamba mbele yake.

Kipa huyu pia alionekana kuwa mwepesi kunyanyuka pindi anapokuwa chini, lakini pia ni mwepesi kuokoa michomo inayopigwa na viungo Frank Domayo na wachezaji wengine wa Azam.

Nahimana alijiunga na KMC msimu uliopita akitokea Vital’O na tangu amejiunga na timu hiyo amejikuta katika mafanikio baada ya kuwa Burundi One na kucheza Fainali za Afrika (Afcon) akiwa kipa namba moja.

Chanzo: mwananchi.co.tz