Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nabi aomba mafaili matatu ya mastaa Yanga

Nabi Pic Data Nabi aomba mafaili matatu ya mastaa Yanga

Tue, 27 Apr 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

WACHEZAJI wa Yanga juzi walikuwa wakicheza kwa mara ya kwanza chini ya ya kocha wao Nesreddine Nabi tangu asaini mkataba wa miezi 18 kuifundisha timu hiyo, lakini kabla ya pambano hilo aliwataka mabosi wa klabu hiyo kumpatia mafaili matatu muhimu ya wachezaji wake.

Inadaiwa jana Nabi ametaka apatiwe faili la wachezaji wote walivyocheza msimu huu akitaka kujua mfano Fiston Abdulrazack amecheza dakika ngapi uwanjani, huku akisisitiza anataka kuwaangalia vijana wake kupitia mechi nne zijazo.

Katika mechi hizo nne ambazo inaelezwa Nabi ametaka kuzitumia kuwasoma vijana wake kabla ya kuwasha moto, ipo pia mechi ya watani wao, Simba itakayopigwa Mei 8 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa pamoja na ile ya Kombe la ASFC itakayopigwa Ijumaa hii.

Kuhusu faili analotaka la wachezaji wake wote, Kocha Nabi anataka pia kujua mechi gani mchezaji alianza na zipi alitokea benchi akiwa na lengo la kutaka kujua kila staa wa kikosi hicho amekuwa na mchango gani.

Faili la pili anataka kujua kila mchezaji amefunga mabao mangapi kwa washambuliaji na kama winga amezalisha mabao mangapi na kama kiungo ametengeneza nafasi ngapi.

Takwimu za mwisho anazotaka ni kadi za njano na nyekundu nani kinara wa kupata kadi na nani amekuwa akikosekana katika adhabu hizo.

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano wa Yanga, Injinia Hersi Said amekiri kuhitajika kwa takwimu hizo akisema atapatiwa haraka.

Hersi alisema katika safari yao ya kwanza kama viongozi kambini kwao walipata nafasi ya kuangalia maandalizi yake na wamegundua ni kocha ambaye ataleta ubora mkubwa kwa wachezaji na timu yao kwa ujumla.

“Ametaka kweli hizo takwimu nafikiri zinafanyiwa kazi kwa haraka ili azipate, amesema anazitaka leo isivuke hapo kuna mambo anataka kufuatilia kuhusu wachezaji,” alisema Hersi na kuongeza;

“Ukiniuliza kipi ameanza nacho naona ni kocha ambaye anakuja kubadilisha ubora wa timu yetu Yanga itakuwa inacheza mpira wa ufundi sana kuanzia jinsi ya kukaba, kushambulia na hata kufunga.”

Hersi alisema kwa namna kocha huyo alivyo ni mtu anayetaka kuitengeneza Yanga ya moto na kusisitiza; “Kwa sasa ameeleza sana akili yake katika kuboresha ufundi na niwaombe Wanayanga wenzangu huu ni wakati wa kutoa nafasi kwa makocha wetu wafanye kazi zao kwa utulivu na tuwape nguvu na sio kuwashambulia.”

“Kwenye mabadiliko kama haya ambayo anataka kuyafanya yanaweza kupokewa kwa haraka na wachezaji au taratibu wakati mwingine, kumleta kocha mapema ili apate muda wa kuyafanyia kazi hayo kwa muda na utulivu.”

Kocha Nabi alikuwepo kwenye pambano dhidi ya Gwambina na Yanga kushinda 3-1 na jana alitarajiwa kukishuhudia kikosi chake kikivaana na Azam FC kabla ya kwenda Sumbawanga Ijumaa kucheza na Tanzania Prisons, kisha kuvaana na Simba Mei 8.

Mechi nyingine Yanga itacheza ni dhidi ya Namungo Mei 15 na ile ya JKT Tanzania itakayochezwa Mei 19 kabla ya ligi kusimama kupisha mechi za kimataifa.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz