Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nabi Ashusha Presha Yanga

YANGA 1.png?fit=820%2C427&ssl=1 Nabi Ashusha Presha Yanga

Fri, 10 Sep 2021 Chanzo: globalpublishers.co.tz

UONGOZI wa Yanga tayari umethibitisha kuwa vibali vya nyota wake wapya watatu, Djuma Shabani, Fiston Mayele na Khalid Aucho vimechelewa kuwasilishwa katika Shirikisho la Soka Afrika (CAF), hivyo kusababisha kuwa na nafasi ndogo kucheza dhidi ya Rivers United ya Nigeria, Jumapili hii.

Licha ya Yanga kuwakosa nyota hao katika mchezo huo wa awali wa Ligi ya Mabingwa Afrika utakaochezwa Uwanja wa Mkapa, Dar, lakini bado uongozi wa klabu hiyo umetamba wana kikosi bora na kipana ambacho kinatosha kuwapa ushindi.

Jeuri ya viongozi wa Yanga imekuja baada ya kuhakikishiwa hivyo na kocha mkuu wa kikosi hicho, Nasreddine Nabi raia wa Tunisia ambaye amekuwa na vijana hao kwenye maandalizi makali tangu Morocco hadi wanarudi Dar kuendelea na maandalizi ya msimu wa 2021/22.

Kuelekea katika mchezo huo, Msemaji wa Yanga, Haji Manara, alisema: “Licha ya kuwakosa wachezaji hao watatu ambao ni muhimu, lakini bado wachezaji ambao watasalia wataweza kuipa ushindi Yanga katika mchezo wetu huo, hivyo Wanayanga msiwe na presha, kila kitu kitakuwa sawa.

”Kukosekana kwa Djuma ambaye hucheza zaidi katika eneo la beki wa kulia, nafasi yake itazibwa vizuri na Kibwana Shomari.

Kwa upande wa Aucho ambaye alionekana kuja kuanza sambamba na Mukoko Tonombe katika eneo la kiungo mkabaji, nafasi yake itachukuliwa na Yanick Bangala Litombo ambaye katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Zanaco alicheza eneo hilo.

Mayele anayecheza nafasi ya ushambuliaji, kukosekana kwake itamfanya Heritier Makambo kutawala eneo hilo muda wote.Kikosi cha Yanga katika mchezo huo kinatarajiwa kuwa hivi; Diarra Djigui, Kibwana Shomari, Adeyum Saleh, Dickson Job, Bakari Mwamnyeto, Yannick Bangala Litombo, Mukoko Tonombe, Feisal Salum, Jesus Moloko, Yacouba Songne na Heritier Makambo.

Chanzo: globalpublishers.co.tz