Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

#NBCLIGIREVIEW: Tazama magoli yote, Ruvu Shooting vs Yanga (+Video)

Video Archive
Tue, 4 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mabingwa watetezi, Yanga SC wameibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Ruvu Shooting katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara usiku wa jana Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Mabao ya Yanga yamefungwa na kiungo Feisal Salum Abdallah dakika ya 52 na beki na Nahodha, Bakari Nondo Mwamnyeto dakika ya 71, wakati la Ruvu Shooting limefungwa na beki Rolland Msonjo dakika ya 86.

Kwa matokeo hayo, Yanga wanafikisha pointi 13, ingawa wanabaki nafasi ya pili nyuma ya watani, Simba SC wanaoongoza kwa wastani mzuri tu wa mabao baada ya wote kucheza mechi sita.

Kwa upande wao, Ruvu Shooting wanabaki na pointi zao tisa za mechi sita pia nafasi ya nne.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live