Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mzungu akunwa kiwango wanariadha Tanzania

24549 Pic+wanariadha TanzaniaWeb

Wed, 31 Oct 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Viwango bora vya wanariadha walioshiriki mbio wazi za Filbert Bayi (FBF), vimemvutia aliyewahi kuwa kocha mkuu wa timu ya Taifa ya riadha iliyoshiriki Olimpiki 1980, Ron Davis.

Akizungumza Dar es Salaam, Davis alisema wanariadha wanariadha walioshiriki mbio hizo wana nafasi ya kufanya vyema katika mashindano ya kimataifa endapo wataungwa mkono.

Davis raia wa Marekani alihudhuria mbio hizo juzi zilizolenga kuwaweka fiti wanariadha wa Pwani kujiandaa na mchujo wa kutafuta tiketi ya kuwakilisha mkoa wao kwenye mashindano ya Taifa yatakayofanyika Dar es Salaam Novemba 16 na 17.

Kocha huyo alisema umri wa wanariadha hao na muda wanaokimbia unatoa taswira njema kuwa wana nafasi ya kushiriki vyema mashindano ya kimataifa.

Mashindano hayo yaliandaliwa na Taasisi ya Filbert Bayi (FBF) yalishirikisha wanariadha wa shule hiyo, klabu ya Nyumbu, Miembe Saba, Pangani Sekondari na wanariadha binafsi.

"Muda waliokimbia vijana hawa ni rafiki, unatoa taswira nzuri kama watapata hamasa na sapoti kidogo, watafanya vizuri kimataifa," alisema kocha huyo raia wa Marekani ambaye amewahi kufundisha nchi za Afrika ikiwemo Tanzania mwaka 1979 na kuiongoza kutwaa medali mbili za Olimpiki 1980.

Katika mbio za mita 100, Abdallah Faudh wa FBF aliibuka kinara akikimbia kwa sekunde 12.95, mwanariadha wa Klabu ya Nyumbu, Godfrey Maulid alikimbia kwa sekunde 13.42 akimaliza kwenye nafasi ya pili na Shabani Masoud pia wa Nyumbu akihitimisha tatu bora akitumia sekunde 14.44.

Katika mbio za mita 400 za wasichana, wanariadha wa FBF walitwaa medali zote wakiongozwa na Regina Mpigachai aliyekimbia kwa sekunde 61.04, Pili Mipawa sekunde 61.08 na Helemengilda Nkululey sekunde 62.07.

Katika mbio za mita 1200 za wavulana, Atson Mbughi wa Nyumbu aliibuka kinara akikimbia dakika 3:11.07, Moses Chacha wa Pangani Sekondari dakika 3:42.05 alitwaa nafasi ya pili na Michael Matson wa Miembe Saba alihitimisha tatu bora akikimbia kwa dakika 4:02.44.

Kwa wasichana, Dorcas Boniface wa FBF aliyekimbia kwa dakika 3:48.84 aliibuka kinara huku Esther Martin pia wa FBF akitwaa medali ya pili ya fedha akikimbia kwa dakika 3:49.46.

Mwenyekiti wa mashindano na mwanariadha nyota wa zamani wa riadha, Filbert Bayi alisema mashindano hayo yana lengo la kuwapima wanariadha wa mkoa kujiweka vyema kwa mashindano ya kitaifa na kimataifa.

Chanzo: mwananchi.co.tz