Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mziba, Mayay wafunguka Makambo kuuzwa Guinea

58281 Pic+makambo

Mon, 20 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Siku chache baada ya mshambuliaji wa Yanga, Heritier Makambo kudaiwa kutia saini mkataba wa miaka mitatu kuitumikia Horoya ya Guinea, wadau wa soka nchini wametoa maoni.

Wakizungumza Dar es Salaam jana, baadhi ya wadau walisema uongozi wa Yanga unapaswa kufungua milango kwa wachezaji wengine hasa vijana kufuata nyayo za Makambo.

Wadau hao walisema wachezaji wanapaswa kuzitumia Simba, Yanga au Azam na timu nyingine kupata mafanikio kucheza soka ya kulipwa nje ya nchi.

“Bahati nzuri uongozi wa Yanga hawana tatizo kuuza mchezaji kama ilivyokuwa zamani wachezaji walikuwa wakibaniwa kutoka,” alisema kocha Kenny Mwaisabula.

Mchambuzi Ally Mayay alisema soka la sasa ni biashara, hivyo kinachotakiwa ni klabu kunufaika inapouza mchezaji kama ilivyotokea kwa Makambo.

Nyota huyo wa zamani wa Yanga, alisema Makambo ameuzwa kipindi kizuri ambacho usajili unakaribia hivyo wasajili mchezaji mwenye kiwango bora kama au zaidi ya Makambo.

Pia Soma

“Unapokuwa na mchezaji wa aina ya Makambo, unapaswa kuwa na Plani B, ikitokea ameondoka, mbadala wake atakuwa nani? Lakini Makambo ameondoka kipindi kizuri,” alisema Mayay.

Nyota wa zamani Yanga, Abeid Mziba alisema kuuzwa Makambo kumedhihirisha uimara wa Yanga katika kuuza wachezaji na kuachana na mfumo wa zamani kuwa mchezaji kama Makambo akiondokana nani ataziba pengo lake.

Mwenyekiti wa zamani wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Kanali Idd Kipingu alishauri Yanga kuanza kuwatengeneza vijana na kuwauza nje kwa kuwa watakuwa msingi mzuri tangu wakiwa wadogo.

Mwenyekiti wa Yanga Dk Mshindo Msolla alisema Makambo atainufaisha klabu hiyo endapo mpango huo utakamilika kwa kuwa ana mkataba wa mwaka mmoja zaidi.

“Mchezaji yeyote atakayepata timu nje ya nchi, klabu haitamgomea kuondoka ilimradi tu na sisi tunufaike na usajili wake,” alisema Msolla ambaye pia ni kocha.

Chanzo: mwananchi.co.tz