Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwandila: Tulieni Makambo, Ajibu mbona mtawasahau

69814 Mwandila+pic

Mon, 5 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

KOCHA Msaidizi wa Yanga, Noel Mwandila amewatoa wasiwasi wapenzi wa timu hiyo kwa kuondokewa na nyota wengi waliovuma msimu uliopita kwenye Ligi Kuu Bara.

Mara baada ya kuwasili juzi Ijumaa wakitokea Morogoro walikokuwa wameweka kambi ya wiki mbili kujiandaa na michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika pamoja na Ligi Kuu, Mwandila amesema hana wasiwasi na kikosi chake.

Amesema kuondoka kwa wachezaji kama, Heritier Makambo na Ibrahim Ajibu hakutawayumbisha kwani wamefanya usajili wa maana timu hiyo na watafanya mambo makubwa.

"Kila timu imefanya mabadiliko ya kuimarisha kikosi chake kwa kusajili wachezaji, ndio maana wengine wameondoka na wengine wamekuja na hakuna anayejua nini kitatokea kwa wachezaji waliosajiliwa msimu huu."

"Kambi ilikuwa nzuri na kikubwa tumewaandaa wachezaji kisaikolojia na utimamu wa mwili 'Physical fitness' na mchezo wa leo Jumapili dhidi ya Kariobangi Sharks utasaidia zaidi kujua ubora wa timu yetu kuelekea mchezo dhidi ya Township Rollers," alisema Mwandila.

Msimu uliopita Ajibu aliyetua Simba, alitengeneza nafasi za mabao 'assists' 17 na kufunga mabao sita kwenye Ligi Kuu huku Makambo akitupia nyavuni mabao 17 na sasa ametimkia  kikosi cha Horoya ya Guinea.

Pia Yanga dakika za mwisho imemtema, Klaus Kindoki nafasi yake imechukuliwa na David Molinga 'Ndama' akitua kwa mkopo akitokea Klabu ya Renaissance, klabu ambayo Makambo aliwahi kuichezea.

Nyota wengine waliotua Jangwani ni pamoja na Patrick Sibomana, Issah Bigirimana, Metacha Mnata, Farouk Shikalo, Seleman Mustafa, Mapinduzi Balama, Lamine Molo, Muharami Issa 'Marcelo', Sadney Urikhob, Maybin Kalengo, Juma Balinya, Ally Sonso na Ally Ally.

Chanzo: mwananchi.co.tz