Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwanasoka mwingine amelamba kitita cha Milioni Moja kutoka Vodacom

2034 Image1 660x400.png

Sun, 28 Jan 2018 Chanzo: millardayo.com

Mshambuaji wa Mbao FC ya Mwanza, Habib Kiyombo amekabidhiwa kitita cha Tsh Milioni 1, Tuzo na king’amuzi kwa kuibuka Mchezaji Bora wa mwezi December  wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) Tanzania Bara msimu wa 2017/2018.

Habib amekabidhiwa zawadi hizo na Afisa Udhamini na Matukio wa Vodacom Tanzania, Ibrahim Kaude na Meneja Fedha wa Bodi ya Ligi, Ibrahim Mwayella ikiwa ni dakika chache kabla timu yake haijaingia uwanjani kupambana na timu ya Ruvu Shootings ya mkoani Pwani.

Huyu anakuwa mchezaji wa pili mzawa kushinda tuzo ya mchezaji bora baada ya Mudathir Yahya kiungo wa Singida United kushinda tuzo ya mchezaji bora wa VPL 2017/2018 kwa mwezi November.

Tuzo hii hapo awali ilikuwa ilichukuliwa na wachezaji wanaotoka nje ya Tanzania ambapo Mwezi August mshindi alikuwa ni Emmanuel Okwi wa Simba, September akawa ni Shafik Batambuze wa Singida United na mwezi October alishinda Obrey Chirwa wa Young Africans.

Daa!! huu utani mwingine “Kama kuna mchezaji ananiacha hoi basi Chirwa”-Manara



 
Chanzo: millardayo.com