Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwanariadha wa Ethiopia avunja rekodi ya Dunia Berlin Marathon

Skynews Tigst Assefa Berlin Marathon 6296655 Mwanariadha wa Ethiopia Tigist Assefa

Mon, 25 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanariadha wa Ethiopia Tigist Assefa Jana Jumapili amevunja rekodi ya Wanawake kwenye Berlin Marathon na vilevile kushinda katika mbio hizo.

Assefa (29) ambaye pia alishinda mwaka jana, aliuvuka mstari wa ushindi baada ya kutumia masaa 2 dakika 11 na sekunde 53, 2:11.53

Mwanariadha huyo ambaye alianza mashindano ya Marathon mwaka jana amevunja rekodi iliyowekwa na Mwanariadha wa Kenya Brigid Kosgei mwaka 2019 ya 2:14.04

Kabla ya kuingia kwenye Marathon Assefa alikuwa mtaalamu wa mita 800.

Bingwa mara mbili wa Olimpiki Eliud Kipchoge (38) ameongoza kwa upande wa wanaume kwa mara ya tano huko Berlin kwa muda wa 2:02.42

Chanzo: www.tanzaniaweb.live