Chama cha Riadha Kenya bado kina mshtuko kufuatia kifo cha aliyekuwa bingwa wa Seoul Marathon, Frankline Chepkwony, kilichotokea Jumatatu asubuhi.
Chepkwony, mwanariadha mzoefu wa mbio ndefu, alianguka na kufa alipokuwa akirejea nyumbani kutoka kwa mbio zake ndefu huko Moringwo, Eldama Ravine katika Kaunti ya Baringo.
Mjomba wakeke, Joseph Tele, amesema kuwa mwanafunzi wa mwanariadha huyo alijaribu kutoa huduma ya kwanza baada ya Chepkwony kuzimia, kabla ya Msamaria Mwema kumkimbiza katika Hospitali ya Eldama Ravine ambapo alitangazwa kuwa amefariki.
“Nilipigiwa simu alipokimbizwa hospitali kwa bahati mbaya alifariki dunia. Sasa tunapanga maziko yake. Tutatangaza tarehe ya maziko mara tu tutakapo kubaliana na familia," Tele amesema.
Mike Boit, ambaye ni mshiriki mwenza wa marehemu Chepkwony katika mazoezi, amesema kuwa siku ya Jumatatu asubuhi, walikuwa na programu ya kukimbia takriban kilomita 23 na walifanya mazoezi ya kupasha mwili joto kabla ya kuachana.
“Programu yetu iliendelea vizuri na alikuwa na ari wakati wa mafunzo. Nilipigiwa simu nilipofika nyumbani kwamba rafiki yangu alikuwa ameanguka na sikuamini. Nilikimbia kwenda nyumbani kwake ambapo nilithibitisha kuwa hayupo tena,” amesema Boit, mwanariadha wa mbio za marathoni.
Chepkwony alikimbia katika mchezo wake wa kwanza wa kimataifa kwa ushindi katika mbio za Zurich Marathon za 2012 baada ya kutumia muda wa 2:10:57 kabla ya kumaliza wa pili kwenye mbio za Eindhoven Marathon, ambapo alitumia muda wake bora zaidi wa 2:06:11 baadaye mwaka huo.
Alishinda Seoul Marathon 2013 kwa saa 2:06:59, kisha akashika nafasi ya saba kwenye Marathon ya Amsterdam ya 2013 akitumia saa 2:09:53.
Alianza kwa mara ya kwanza katika mbio za Dunia za Marathon 2014, na kumaliza wa tatu katika mbio za Boston Marathon katika mbio alizoshinda Meb Keflezighi wa Marekani. Wilson Chebet wa Kenya alikuwa wa pili.
Aliyekuwa mshikilizi wa rekodi ya dunia ya mbio za marathoni Dennis Kimetto, ambaye alizoea kufanya naye mazoezi katika Kapng’etuny huko Ainabkoi, Kaunti ya Uasin Gishu, aameshtuka kupata habari kuhusu kifo cha Chepkwony.
"Alikuwa mwanariadha mnyenyekevu ambaye kila wakati alipenda kufanya kazi kama timu. Inasikitisha sana kwamba imebidi afe kwa namna hiyo. Tutamkosa,” alisema Kimetto. Mwili wake umehamishiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti ycha Hospitali ya Eldama Ravine.