Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwanariadha Mtanzania akamata nafasi ya Tatu Berlin Marathon

Shauri Berlin Marathon.jpeg Mwanariadha wa Tanzania, Magdalena Shauri

Mon, 25 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanariadha wa Tanzania, Magdalena Shauri ambaye alikuwa mshindi wa Dodoma NBC half Marathon 2023 ameandika historia mpya katika maisha yake baada ya kushika nafasi ya tatu katika mashindano ya #berlinmarathon kwa kilometa 42 akitumia saa 2:18:41.

Mashindano hayo yametimua vumbi siku ya Jana Septemba 24, 2023 nchini Ujerumani huku Magdalena akitanguliwa na Tigist Assefa kutoka Ethiopia aliyemaliza wa kwanza kwa saa 2:11:53 na Mkenya Sheila Chepkirui aliyemaliza nafasi ya pili akitumia saa 2:17:49.

Magdalena ambaye alikuwa akichuana na wakimbiaji mashuhuri duniani kutoka Ethiopia, Kenya, Marekani, Uganda, Uingereza na nchi nyingi duniani akimaliza nafasi ya tatu na kujikatia tiketi ya kushiriki michuano ya Olympic itakayofanyika Paris nchini Ufaransa mwakani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live