Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwanariadha Mkenya ampa Chipukizi vifaa vya Michezo

Athletes Mwanariadha Chipukizi, Jeanine Keazimana akipokea vifaa vya michezo kutoka kwa Mary Moraa

Tue, 24 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanariadha Chipukizi wa Burundi, Jeanine Keazimana amepokea msaada wa vifaa vya michezo kutoka kwa Mwanariadha wa Kenya Mary Moraa.

Hatua hiyo imekuja baada ya Chipukizi huyo kuonekana akishiriki katika mbio za Wanawake za mita 3000 wakati wa Mashindano ya riadha ya dunia ya vijana chini ya miaka 20.

Chipukizi huyo alikosa viatu vinavyostahii kutumika katika mashindano hayo, ila kutokana na mapenzi yake katika mchezo huo, Keazimana alishiriki kwa kuvaa raba kukuu na kumaliza katika nafasi ya 10 huku Mkenya Teresia Muthoni akiibuka mshindi.

Mwanariadha huyo chipukizi aligonga vichwa vya habari kwa kushiriki mashindano bila viatu vinavyotumika katika michezo ya riadha.

Tukio hilo lilimsababisha mwanariadha huyo wa olimpiki wa mita 800 kumzawadia Keazimana jezi nzima ya vifaa vya riadha.

"Tulikuwa tukitazama mbio kutoka stendi na nilihisi vibaya sana kumuona akianguka karibu mara tatu kwenye mbio. Viatu ambavyo alikuwa amevaa havikuwa bora kabisa kukimbia. Kama mwanariadha, nilihisi uchungu," Moraa ameiambia Capital FM.

Kwa upande wake kocha wa Moraa, Isaac Too amemzawadia Mwanariadha huyo chipukizi viatu vya Nike.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live