Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwamuzi atelekeza wachezaji uwanjani akikimbia nyuki

56298 Pic+mwamuzi

Wed, 8 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

TABORA. PAMBANO la soka la Kombe la Mbuzi  kati ya Black Mamba na Mfupa wa Mamba baada ya mwamuzi wa mchezo huo Benedicto Elisha kuamua kutimua mbio ghafla huku akiwaambia wachezaji wa timu hizo kukimbia baada ya kundi la Nyuki kuibuka ghafla uwanjani hapo.

Mchezo huo wa ufunguzi ulipigwa katika Uwanja wa Itundu ambapo nyuki hao waliibuka ghafla dakika ya 10 uwanjani hapo na kuzua kizazaa hicho kilichofanya kila mtu akimbie kinyake kuokoa maisha yake.

Baada ya dakika 20 za utawala wa nyuki hao ndipo Mwamuzi Elisha alirejea uwanjani hapo na mchezo huo kuendelea huku wakicheza kimachale kuhofia wadudu hao kama wanaweza kurudi tena.

Mchezo huo uliendelea ambapo Black Mamba waliweza kupata ushindi wa mabao 2-0 katika mpambano huo uliojaza mashabiki wengi uwanjani hapo.

Black Mamba walipata bao la kuongoza dakika ya 27 ambalo lilipachikwa nyavuni na Mshambuliaji David Ally kisha Moses Arbogasti kupachika la pili dakika ya 89.

Mratibu wa Ligi hiyo,Shaban Kapondya alisema Mashindano hayo yanashirikisha timu Nane kutoka ndani ya Wilaya ya Urambo ambapo lengo lake ni kuibua na kuendeleza vipaji vya soka.

“Tumezigawanya katika makundi mawili zenye timu Nne ambapo zitacheza na badaye kuja kutoa mbili kila mmoja kisha kucheza Nusu fainali,”alisema Kapondya.



Chanzo: mwananchi.co.tz