Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwamuzi afariki dunia baada ya kupokea simu mechi ikiendelea

65372 Pic+mwamuzi

Thu, 4 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Serengeti. Katika hali ya kushangaza mwamuzi Gugumiya Werema (30) amekufa ghafla wakati akichezesha mpira kati ya Nyakitono fc dhidi ya Nyanungu Fc wilaya ya Serengeti mkoa wa Mara.

Afisa mtendaji wa kata ya Kyambahi, Mohammed Salum akizungumza na Mwananchi kwa simu leo Jumatano Julai 3, 2019, amesema tukio hilo limetokea jana Julai 2 muda mfupi baada ya mwamuzi huyo kupigiwa simu.

Salum alisema wakati mchezo ukiendelea alipokea simu, ghafla wakaona anaishiwa nguvu na kuanguka, kumkimbiza kituo cha Afya Natta akawa ameishafariki.

Katibu wa hospitali Teule ya Nyerere, Mboha Kazare amethibitisha kupokelewa kwa mwili wa Werema kwa maelezo kuwa alipokea simu akafa, hata hivyo amedai uchunguzi wa kujua chanzo cha kifo ndugu wakihitaji.

Kamanda wa Polisi wilaya ya Serengeti, Methaw Mgema alisema hakuna mtu aliyetoa taarifa kuhusiana na tukio hilo na kuwa wako tayari kufanya uchunguzi kuhusiana na madai ya simu kusababisha kifo iwapo watajitokeza watu.

Chanzo: mwananchi.co.tz