Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwamuzi Simba na Yanga utata mtupu, mwenyekiti wa kamati, Salum Chama atoa ufafanuzi

7154 DSC0596 TZW

Sun, 29 Apr 2018 Chanzo: bongo5.com

Imekuwa ni kawaida kila kunapokaribia mchezo wa watani wa jadi Simba SC na Yanga SC kujitokeza kwa utata ambapo hivi sasa kunamalalamiko kwa baadhi ya watu kudai uhalali wa mwamuzi wa mtanange huo, Emmanuel Mwandembwa kutambuliwa na TFF kuwa anatoka Mwanza ilihali yeye ni mtu wa Arusha swala ambalo Mwenyekiti wa Kamati ya Waamuzi, Salum Chama analitolea ufafanuzi.



Mwenyekiti wa Kamati ya Waamuzi, Salum Chama

Kupitia kipindi cha michezo cha radio Efm, Salum Chama ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Waamuzi ndani ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF amesema kuwa Kamati ya waamuzi ndiyo yenye mamlaka ya kupanga waamuzi na ndiyo inayo panga kama kuna mtu mwenye ushahidi wowote aufikishe mezani kwake.

Kamati ya waamuzi ndiyo yenye mamlaka ya kupanga waamuzi na ndiyo inayo panga kama mtu anao ushahidi wowote unaosema kwamba huyu anahusika basi autoe hadharani.

Lakini ninachofahamu sisi tunapokutana tunapanga waamuzi na kunawakati tunafanya marekebisho kulingana na uzito wa mchezo na wakati mwingine tunafanya marekebisho kulingana na uwezo kwahiyo kunapofanyika mabadiliko usichukulie kwamba kunamtu anashinikiza, mimi siyo mtu wa kushinizwa nina misimamo mikali na ninajisimamia kabisa.

Hakuna mtu ndani ya kamati anaeshinikiza nani apangwe, hilo jambo mimi sijaliona na wala sikweli sasa kama kunamtuanapanga nafikiri wao kama kuna malamiko hayo basi wangeandika barua kwangu na kusema huyu kachezesha 15 na huyu mbili ningekuwa na majibu ambayo yana uhakika lakini wanapo lalamika bila kuleta takwimu linakuwa ni jambo ambalo unashindwa kulitolea maamuzi.

Kwa utendaji wa kamati ya waamuzi ni ule ule tangu mimi nimekuwa mwenyekiti kwenye kipindi kilichopita rais aliyepita ndugu  malinzi na sasa Karia.

Sisi tunafanya kazi zetu kama kamati na kwa maelekezo ya kamati na kwamujibu wa waraka wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani FIFA na CAF.

Mwamuzi, Emmanuel Mwandembwa yeye anatoka Arusha lakini sasa yupo Mwanza katika chuo cha Malya anachukua Diploma pale kwa miaka mitatu sasa utasemaje yupo Mkoani Arusha.

Mtu anachukua Diploma atakuwepo pale kwa miaka mitatu utamtajaje bado yupo Arusha, akimaliza masomo atavaa kofia yake ya Mkoa wa Arusha akitoa taarifa tutamtambua pale atakapo kuwa kwa sababu ya mambo haya ni kwamba mwamuzi anarudishiwa nauli walizotumia katika safari huwezi kumlipa nauli ya Arusha na wakati yupo Mwanza.



Simba SC itakuwa mwenyeji kwenye mchezo huo wa watani wa jadi wakiwakaribisha Yanga SC dimba la uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam Aprili 29.

Vinara wa ligi kuu soka Tanzania Bara Simba itashuka uwanjani huku ikiwa na nia ya kushinda mchezo huo ili kuzidi kujiahakikishia nafasi ya kutwaa ubingwa huo ambao umeukosa kwa takribani miaka mitano sasa huku hasimu wake Yanga ikishuka katika dimba hilo ili kuchomoka na alama tatu muhimu na kuzidi kuwakaribia wapinzani wao katika mbio hizo za Ubingwa.

Chanzo: bongo5.com