Akizungumza baada ya kumalizika kwa mechi hiyo, Mwamnyeto alisema hawajakata tamaa na wanahitaji kupambana hadi mwisho wa ligi ndipo watakapojua nafasi halisi ambayo wapo.
"Mechi ilikuwa ngumu sana. Tulitaka kushinda, lakini kwa bahati mbaya tumetoka suluhu, unajua unaweza kupanga hili, Mungu naye anapanga lake. Hatujakata tamaa sisi tunazidi kupambana tu," alisema.
Kwenye mechi yao dhidi ya Namungo, beki huyo wa zamani wa Coastal Union alisema walicheza vema sana, lakini tatizo kubwa aliloliona ilikuwa kwenye ufungaji tu.
Naye Kocha Mkuu wa Namungo, Hemed Suleiman 'Morocco' alisema walitengeneza nafasi nyingi zaidi kuliko Yanga, lakini walishindwa kuzitumia.